7 Julai 2025 - 23:13
Source: Parstoday
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Russia watungua droni 400 za Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa Jeshi la anga la nchi hiyo limefanikiwa kudungua ndege zisizo na rubani 402 za Ukraine na mabomu saba ya angani yaliyokuwa yakiongozwa tokea mbali.

Wizara hiyo imesema hayo leo Jumatatu na kueleza kuwa, ndege zisizo na rubani 91 ziliharibiwa usiku wa kuamkia leo, nyingi yazo zikiwa katika maeneo ya mpaka ya Belgorod na Kursk, na nane katika mkoa wa Moscow.

Russia na Ukraine zimezidisha mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika siku za hivi karibuni. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Jumatatu kwamba, Russia Urusi ilirusha ndege zisizo na rubani 101 usiku wa jana, na kuongeza kuwa takriban droni 1,270 na makombora 39 yalisajiliwa katika muda wa wiki moja iliyopita.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi wa Russia imesema imesambaratisha hatua za serikali ya Kiev za kutekeleza mashambulizi ya kigaidi kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora ya Tochka- U dhidi ya maeneo mbalimbali katika ardhi ya Shirikisho la Russia. 

Hivi karibuni pia, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema kuwa mifumo yake ya ulinzi wa anga imetungua droni 35 za Ukraine zilizokuwa zikiruka katika majimbo ya Kursk, Voronezh, Belgorod, Bryansk na Oryol huko Russia. 

Tangu Februari 2022, nchi za Magharibi zimeipatia Ukraine silaha na zana mbalimbali za kijeshi ili kusaidia vikosi vya Kiev dhidi ya Russia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha